Friday, October 16, 2015

Mbunge Deo Filikunjombe na baba yake Jerry Silaa wamefariki kwa ajali ya Helikopta.. #RIP

on
Kumekuwa na mvutano wa taarifa zinazoripotiwa kuhusu ajali ya Helikopta iliyotokea jioni ya October 15 2015 katika Msitu wa Mbuga ya Selous, pembeni ya Mto Ruaha.
Jerry INSTA
Jerry Silaa amepost Ujumbe huu akithibitisha kufariki kwa Mbunge Deo Filikunjombe pamoja na baba yake, Mzee William Silaa ambaye alikuwa Rubani wa Helikopta hiyo >>> “Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha…. Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa, nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani— jerrysilaa
Hii ni picha ya zamani, Mbunge Zitto Kabwe akiwa na Marehemu Deo Filikunjombe.
Hii ni picha ya zamani, Zitto Kabwe akiwa na Marehemu Deo Filikunjombe.

Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi. Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr. Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine. JS>>> jerrysilaa
Deo Filikuonjome
Marehemu Deo Filikunjombe na baadhi ya Wapigakura wake wa Jimbo la Ludewa, Mkoa wa Njombe.

Habari kutoka katika blog ya Millard Ayo zinasema Reporter wa millardayo.com amemtafuta Jerry Silaa lakini simu yake ilipokelewa na Msaidizi wake, Fadhili Idd ambaye amesema ni kweli wanethibitishiwa kuhusu taarifa ya Msiba na wanajiandaa na taratibu nyingine kwa sasa.
RIP Marehemu Captein William Silaa & Mbunge Deo Haule Filikunjombe.

Picha na habari hii ni kwa mujibu wa millardayo.com

Friday, October 9, 2015

Kwenye maisha yako uliwahikufikiria mshindano kama haya

www.facebook.com/massyndaro

Umeiona hii ya huyu mwandishi

Taarifa za Rais Kikwete kupewa tuzo ya heshima na Taswa na wanamichezo wengine ipo hapa

By Massy Ndaro October 9, 2015
facebook.com/massyndaro
Ni kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona watu fulani kutoka tasnia fulani kupewa tuzo za heshima kwa kutambua mchango wao katika sekta husika. Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA, kimetangaza rasmi kufanyika kwa tuzo hizo Jumatatu ya October 12 huku mgeni rasmi akiwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Tuzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka kwa mwaka huu zitakuwa tofauti kidogo kwani zitatumika kumuaga Rais Jakaya Kikwete na kumpa tuzo ya heshima kwa kuthamini mchango wake katika kipindi cha miaka 10 aliyokuwa madarakani.
DSC_0119
Awali tuzo hizo zilikuwa zifanyike October 8 ila kwa sasa zitafanyika Jumatatu ya October 12, tuzo zitatolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, baadhi ya tuzo zitakazotolewa siku hiyo ni tuzo 10 za wachezaji bora waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, tuzo 5 kwa viongozi wa michezo, taasisi iliyochangia kukuza michezo katika kipindi cha miaka 10 na tuzo ya heshima kwa Mh Rais.
Mwewnyekiti wa TASWA  Juma Pinto na katibu mkuu wa TASWA Amir Mhandowamethibitisha hayo kufanyika katika mkutano na waandishi wa habari.
“kwa wale ambao hamfahamu tutatoa Tuzo kumi kwa wachezaji wale ambao wamefanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi ila tumeangalia nje ya Tanzania yaani Afrika Mashariki lakini tutatoa tuzo kwa viongozi watano waliochangia kukuza michezo, tuzo zote hizo zitatolewa na Rais Kikwete”>>> Amir Mhando

Thursday, October 8, 2015

Masaa machache baada ya kusimamishwa Sepp Blatter ..huyu ndiye kiongozi mpya wa FIFA!!

By Masogo Ndaro
Masaa machache baada ya Rais wa FIFA Sepp Blatter kusimamishwa kuliongoza shirikisho hilo, kiongozi wa shirikisho la soka Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho hilo kwa muda.
Hayatou atachukua nafasi hiyo kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais huyo wa FIFA kwa muda wa siku 90 na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo.
Hayatou, ambaye aliongoza CAF tangu mwaka 1988, pia alikuwa makamu wa rais katika kamati ya utendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.
Blatter amesimamishwa kwa muda wa siku 90 kufuatia kashfa mpya ambayo imeibuka hivi karibuni ndani ya shirikisho hilo ikihusisha malipo ya fedha ambazo ziliandikishwa kwa akaunti ya rais wa shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya Michel Platinni
Rais mpya wa FIFA atapatikana Februari 26, 2016.

Hii ndio video ya Laptop ya Microsoft...Microsoft Surface Book

Micosoft yatoa Laptop

Sekunde 90 za kushuhudia Laptop ya kwanza ya Microsoft kwenye muundo wa pekee kabisa… (Pichaz & Video)

By Masogo Ndaro
on
Kwa sababu kila mtu anahitaji kuwa na kifaa kizuri cha Mawasiliano, nimeona kuna umuhimu pia uipate na hii mpyampya kutoka Kampuni ya Kampuni ya Microsoft, Marekani.
Microsoft ni kampuni ambayo imewekeza sana kwenye Teknolojia, walianza na biashara ya kutengeneza program za Computer, baadae wakaendelea kukuza biashara yao… mwaka 2014 Microsoft waliamua kuinunua pia Kampuni ya Nokia na kuendelea na Biashara ya uzalishaji wa Simu.
New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
Kipya kinachokuja ni hii laptop mpya, imepewa jina la Microsoft Surface Book, hii ni zaidi ya laptop ya kawaida, ina uwezo wa kutumika kama Laptop au unaitenganisha alafu inakuwa Ipad… hii itakuwa ya kwanza kabisa kutengenezwa na Kampuni hiyo ya Microsoft.
New York City - October 6, 2015 Panos Panay introduces the Microsoft Surface Book at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
Unaambiwa kama ikijaa chaji ina uwezo wa kufanya kazi mpaka kwa saa 12, mpango walionao ni kuitambulisha na kuiingiza rasmi sokoni kuanzia October 26 2015 na itauzwa kwa Dola 1,499 ambazo zinagusa kama Milioni 3.2.
New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
Ukiangalia hata sehemu inapojikunjia imekaa tofauti na nyingine nyingi tulizowahi kuziona mtu wangu.
New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
Iko na video yake pia hapa kwenye sekunde 96.